MESSI ASHEREKEA MIAKA 14 NDANI YA BARCELONA
Messi amefikisha miaka 14 tokea alipojiunga na Barcelona akiwa na
umri wa miaka 13 akitokea kwao Argentina.
Mkali huyo ambaye sasa ana umri wa miaka 27, amesherekea miaka
hiyo 14 mtandaoni kwa kuweka picha ya kitambulisho chake cha kwanza kabisa
Hispania.
Pamoja naye, klabu yake pia iliweka kitambulisho hicho mtandaoni
kama kumbukumbu.
Tayari
Messi ameichezea Barcelona mechi 460 na kushinda makombe sita ya La Liga,
mawili ya Copa de Rey, sita ya Spanish Cup na matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Angalia
data zake
Mechi: 460
Mabao: 367
Makombe:
Spanish League (La Liga): 6
Spanish Cup (Copa del Rey): 2
Spanish Supercup: 6
Champions League: 3
FIFA Club World Cup: 2
UEFA Super Cup: 2
Ballon d'Or: 4
Post a Comment