Membe: Bila kufuli la CCM pasingetosha urais 2015
Uamuzi wa Kamati Kuu ya CCM wa kuwadhibiti kwa
mwaka mmoja makada wake sita waliobainika kukiuka kanuni kwa kuanza
mapema kampeni za urais, unaweza kuwa uliwakera wengi, lakini si Waziri
wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, ambaye ni mmoja wa ‘waliofungwa kufuli’.
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, ambaye ni mmoja wa ‘waliofungwa kufuli’.
Membe anaona adhabu hiyo ilikuwa mwafaka na kwamba laiti uamuzi huo usingefanywa mapema, “ingekuwa vurugu tupu”.
“Sijui nchi hii ingekuwa wapi kama watu wangeachwa
bila ya kuwekewa ‘gavana’,” alisema Waziri Membe kwenye mahojiano
maalumu na gazeti hili yaliyofanyika kwenye ofisi za wizara hiyo jijini
Dar es Salaam wiki iliyopita.
Membe pamoja na makada wengine, Frederick Sumaye,
Edward Lowassa, William Ngeleja, Stephen Wasira na January Makamba
walibainika kukiuka kanuni za uongozi na maadili za CCM kwa kuanza
kampeni za kutafuta kuteuliwa na CCM kugombea urais.
Kwa mujibu wa taarifa ya CCM iliyotolewa baada ya
kikao cha Kamati Kuu, makada hao walikiuka kanuni za uongozi na maadili
za CCM kwa mujibu wa Toleo la Februari 2010 Ibara 6 (7) kwa baadhi yao
kufanya vitendo vinavyokiuka maadili ndani ya jamii.
Bila ya kueleza ni jinsi gani vurugu hizo
zingefanyika, Membe alisisitiza kuwa vurugu ingekuwa kubwa kama chama
hicho kisingechukua hatua mapema.
“We angalia, kuna makundi mawili. Hili kundi letu
(la walioanza kampeni mapema wakaadhibiwa) na hili jipya la hawa ambao
wameanza kujitokeza sasa, ingawa najua nao watadhibitiwa tu. Hawa
wasingedhibitiwa, ingekuwaje?” alihoji Membe.
Wakati CCM inawaita makada hao kwa ajili ya
kuwahoji, tayari baadhi walishaanza kufanya sherehe na kualika wenyeviti
wa mikoa ambao walieleza misimamo yao juu ya mgombea urais wanayemuunga
mkono, wengine kuzunguka kwenye hafla mbalimbali kwa ajili ya harambee
na wengine kuzigawa jumuiya za chama hicho, hasa Umoja wa Vijana
(UVCCM), huku baadhi ya vikao vikiripotiwa kutawaliwa na malumbano
yaliyosababishwa na misimamo tofauti kuhusu mgombea urais wa CCM.
Hata hivyo, Waziri Membe (61) hakusita kukosoa
muundo wa vyombo vya uamuzi vya CCM ambao unawapa fursa baadhi kushiriki
katika kuadhibu wanaotaka nafasi fulani na baadaye walioadhibu
kujitokeza kuwania nafasi hiyo akisema utaratibu huo unawaonea wale
ambao hawana fursa ya kuwadhibiti wengine.
“Chama chetu sasa kiwe na utaratibu unaowabana
watu fulani kugombea kutokana na nyadhifa zao. Kwa mfano, uko kwenye
nafasi ya kufanya uamuzi, unawaadhibu hawa halafu baadaye unajitokeza
wewe. Huwezi kuchuja halafu ukajitokeza wewe (kugombea). Kutakuwa hakuna
objectivity (haki),” alisema bila ya kuweka bayana watu waliohusika
katika kuadhibu na baadaye wakajitokeza kuwania urais.
“Tuwe na utaratibu kwenye chama kwamba wanaowabana
watu fulani, wasigombee na hasa wale walioshiriki uamuzi ule na wengine
walioko kwenye nafasi za uamuzi… Kamati Kuu na hata (Halmashauri Kuu)
Nec na Kamati ya Maadili, nao wasije kujitokeza baadaye na kutangaza
nia. Vinginevyo hatutawaelewa,” alisema.
Pamoja na kusifu kitendo cha Kamati Kuu kudhibiti
makada mapema, Membe anaona muda umefika kwa CCM kuruhusu wanachama wake
wanaowania urais waanze harakati zao sasa.
SOURCE: MWANANCHI
SOURCE: MWANANCHI
Post a Comment