Header Ads

EXCLUSIVE--KIPIGO CHA WAANDISHI JANA, JUKWAA LA WAHARIRI WACHARUKA, SOMA WALICHOKISEMA MUDA HUU

      Siku moja baada ya  sakata la waandishi wa habari kupokea kipigo wakati wakiwa eneo  kazi makao makuu ya polisi jana,jukwaa la wahariri Tanzania(TEF) limeibuka na tamko nzito la kulaani kitendo hicho kwa kile walihodai kuwa ni mwendelezo wa kuendelea kuwaadabisha wanahabari wakati wakitekeleza majukumu yao.
 
       
Hayo yamesemwa mda huu Jijini Dar Es Salaam na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini (TEF)Absalom Kibanda wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo Kibanda alisemwa wao Jukwaa la Wahariri wamesikitishwa kitendo cha Kinyama walichofanyiwa Waandishi wa habari wakati wa wakati wakitekeleza majukumu yao ya kawaida.
“sisi kama jukwaa la wahariri tumesikitika sana kwa kile kitendo cha jana na huu ni mwendelezo wa matukio ya kutembeza vipigo kwa wanahabari wakati wakiwa katika maeneo yao ya kazi”amesema kibanda.
            Aidha jukwaa hilo limewataka jeshi la polisi kufanya mambo kadhaa kabla ya jukwaa hilo halijachukua hatua zaidi ambapo kati ya mambo hayo ni pamoja na kuwakamata mara moja askari watatu ambao wanaonekana katika picha wakimshambulia mwandishi wa gazeti la Tanzania daima Josephat isango.
          
MWANDISHI WA HABARI WA GAZETI LA HOJA SHAMIM AUS AKIWA NA JERAHA SEHEM ZA USONI BAADA YA KURUPUSHANI ZILIZOTOKEA NA KUANGUKA CHINI BAADA YA KUFUKUZWA NA POLISI
 
Pia wamelitaka jeshi la polisi kufanya ukaguzi wa elimu na uwezo wa askari wao kwa kile alichosema kuwa kama askari anatambua majukumu yake ya kazi hawezi kufanya kitendo cha kinyama kama kile cha jana kwa wanahabari hivyo wanamtaka mkuu wa jeshi la polisi kuhakikisha wanafanya usafi kwa askaria ambao hawana sifa ndani ya jeshi hilo.


  Katika tukio la jana jeshi la polisi kwa kupitia askari wake walijikuta wakiwashambulia wanahabari bila kujulikana sababu mara moja ambapo wanahabari kadhaa walidhurika.

No comments

Powered by Blogger.