Chelsea yazidi kujiimarisha, Kagawa arejea Dortmund
Shinji Kagawa akikabidhiwa uzi wake mpya wa Dortmund baada ya kuondoka Manchester Utd |
KLABU
ya Chelsea imezidi kujiimarisha baada ya kukamilisha uhamisho wa Loic
Remy kwa dau la Pauni Milioni 8 kutokaq QPR, huku Mjapan Shinji Kagawa
wa Manchester United akirejea klabu yake ya zamani ya Borrusia Dortmund.
Remy
aliyekuwa anatakiwa pia na Arsenal, anakwenda kuziba nafasi ya Fernando
Torres aliyehamia AC Milan kwa mkopo wa muda mrefu.
Uhamisho
huu ni faraja kwa Remy ambaye sasa anakwenda kujiunga na klabu
inayocheza Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kocha Mreno, Jose Mourinho alihitaji
mshambuliaji baada ya kumtoa kwa mkopo Torres.Katika kuelekea mwisho wa kufungwa kwa dirisha la usajili barani Ulaya, Shinji Kagawa ambaye hakuwa akipewa nafasi kubwa ndani ya Mashetani WEkundu amerejea Ujerumani kuichezea Dortmund.
Kiungo huyo amerejea Dortmund kwa dau la Pauni Milioni 6.3, miaka miwili tu tangu aondoke klabu hiyo ya Ujerumani.
Kagawa atasaini Mkataba wa miaka minne na Dortmund, ambayo ilimuuza Mjapani huyo United mwaka 2012 kwa Pauni Milioni 12.
Remy akisaini mkataba wa kujiunga na Chelsea |
Akionyesha uzi mpya wa klabu yake ya Chelsea |
Post a Comment