YAYA TOURE AOMBA RADHI MAN CITY KWA KADI NYEKUNDU
MWANASOKA bora wa Afrika, Yaya Toure amewaomba radhi wapenzi wa Manchester City kwa kadi nyekundu aliyopewa jana kwenye mechi na CSKA Moscow, wakifungwa
2-1.
Toure alikuwa mchezaji wa pili wa City kutolewa nje katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Etihad, kufuatia Fernandinho
kutolewa mapema.
Nyota huyo wa Ivory Coast aliifungia timu ya Manuel Pellegrini bao la kusawazisha kwa mpira wa adhabu, kabla ya Seydou Doumbia kufunga kwa mara ya pili, kuipatia timu ya Urusi bao la ushindi.
Toure ametweet: "Mashabiki wa City- Samahani kwa kadi yangu nyekundu. Nafikiri
ni muhimu kuomba radhi kwa hili,".
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31, awali alitweet: "Siku ya Mchezo... #Fuatilia'.
City sasa inashika mkia kwenye kundi katika kuwania kucheza hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa na Pellegrini lazima ashinde dhidi ya Bayern Munich nyumbani kabla ya kwenda kupambana ugenini na Rome katika mchezo wa mwisho.
Post a Comment