Header Ads

Vengu wa Orijino Komedi Yaanza kuimarika, Kumbukumbu zaanza kurejea, apewa jumba la milioni 120

Msanii staa wa Kundi la Orijino Komedi ‘OK’, Joseph Shamba ’Vengu’ ameanza kurejea katika
‘fomu’ baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa ndugu wa karibu wa msanii huyo , Vengu ambaye kwa muda mrefu alipoteza kumbukumbu kiasi cha kushindwa kuwatambua watu, sasa amejaliwa kwani anaweza kuwafahamu watu mbalimbali wanaopata nafasi ya kwenda kumjulia hali, Kigamboni jijini Dar anakoishi.

“Bado yupo chini ya uangalizi maalum wa kifamilia, ni watu wachache wanaruhusiwa
kumuona, lakini sasa hivi huwezi kuamini, watu wanaofika kumtazama anawatambua na anawapa ‘hi’."

Kutokana na usiri wa hali ya msanii huyo unaofanywa na familia yake, kumekuwa na
maneno chini kwa chini ikiwa ni pamoja na uzushi wa mara kwa mara kuwa, mchekeshaji huyo maarufu, amefariki dunia na kuzikwa kwa siri
jambo ambalo si la kweli.

Hata hivyo, katika namna ya kusikitisha, ndugu huyo alisema kuwa kila Vengu anapomtambua
mtu anayemtembelea amekuwa akimwaga machozi hali inayoonesha kuwa anarejesha nyuma kumbukumbu zake na kugundua amekuwa
mbali naye kwa muda mrefu.

Pia ndugu huyo alisema kwa hali ya Vengu sasa anaweza kurejea kwenye kazi zake za kuchekesha
kama zamani zile.

No comments

Powered by Blogger.