Header Ads

Ukweli Kuhusu: Mfanyabiashara Kufariki Akifanya Mapenzi Ndani Ya Gari - Kagera

Polisi mkoani Kagera inachunguza kifo cha mmiliki wa ukumbi wa klabu ya usiku ya Linas
Night, Leonard Mtensa (50) ambaye inadaiwa alifariki dunia wakati akifanya mapenzi kwenye gari lake.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe alisema Mtensa, ambaye alikuwa na mpenzi wake kwenye gari maeneo ya Buyekera, alifariki dunia kabla ya kufikishwa kituo cha afya cha ELCT Ndolage.

Alisema binti waliyekuwa naye kwenye gari anatokea mkoani Mara na kwamba tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana.

Hata hivyo, Alisema baada ya gari lake kupekuliwa, vilikutwa vinywaji
mbalimbali.

“Baada ya upekuzi ndani ya gari lake, vilikutwa vilevi vya aina mbalimbali, ikiwamo whisky aina
ya Bond 7 aliyokuwa anakunywa, lakini chanzo cha kifo hicho hakijajulikana,” alisema
Mwaibambe.

Aidha, Kamanda Mwaibambe alisema polisi wanamshikilia mpenzi wake kwa ajili ya upelelezi kwa hatua zaidi.

Kifo hicho kimeshtua wakazi wa
Bukoba, kutokana na mazingira ya kifo cha mfanyabiashara huyo anayemiliki ukumbi pekee mjini hapa unaotoa burudani hadi asubuhi.

Picha za Marehemu, aliyekuwa mpenzi na maelezo ya Kamanda wa Polisi Kagera yapo chini.

No comments

Powered by Blogger.