Header Ads

Picha za Uchi: Desire Luzinda Aomba Radhi

Kufuatia kusambaa kwa picha za utupu za msanii wa muziki Desire Luzinda kutoka nchini Uganda, msanii huyu amechukua hatua ya kuomba msamaha kwa tukio hili la aibu kwake.

Desire katika waraka mfupi wa msamaha alioandika, amewataka radhi mama yake mzazi, mwanae wa kike, familia yake marafiki na mashabiki wake na kuwataka kufahamu kuwa, kuvuja kwa picha hizi kumetokana na kuvunjika kwa uaminifu kutoka kwa mtu aliyempenda akiwa na nia ya kutaka kumharibia maisha sasa.

Msanii huyu amesema kuwa, anakubali kubeba lawama zote kutokana na tukio hili la aibu huku akiweka wazi kuwa juhudi zinafanywa na vyombo vya usalama kuhakikisha kuwa haki inatendeka katika hili.

No comments

Powered by Blogger.