Header Ads

Waumini washambuliwa Jerusalem

Takriban waisreli wanne wameuawa na wengine 8 kujeruhiwa katika kile polisi wanasema ni shambulio la kigaidi dhidi ya Sinagogi eneo la
magharibi ya Jerusalem.

Polisi inasema wanaume waliojihami kwa visu na mapanga wanaoshukiwa kuwa Wapalestina ndio waliofanya mashambulizi hayo.
Washambuliaji wawili wamepigwa risasi na kuuawa.

Israel imekuwa katika hali ya tahadhari kuu baada ya mashambulio kadhaa na Wapalestina wakizozana na Waisraeli kuhusiana na eneo
takatifu ambalo wamekuwa wakizozania.

Vyombo vya habari nchini Israel vinasema kuwa ufyatulianaji risasi ulitokea kati ya polisi na washambuliaji hao waliowasili katika eneo hilo pindi taharuki ilipozuka.

Msemaji wa polisi alieleza kwamba eneo la mashambulizi lilizibwa na kwamba waliojeruhiwa wakiwemo waumini sita na polisi wawili, walipokea matibabu katika hospitali mjini Jerusalem.

Watu wengine wanne wanasemekana kuwa hali mahututi na kwamba mshambuliaji wa tatu huenda ametoroka.

Hali ya wasiwasi imekuwa ikikumba mji huo katika wiki chache zilizopita huku kukitokea mashambulizi makali yaliyofanywa na wapiganaji
wa kipalestina dhidi ya raia waliokuwa wanatembea mjini.

Pia kumekuwa na wasiwasi kuhusu mpango wa Israel kujenga makazi zaidi ya walowezi eneo la
Mashariki mwa Jerusalem.

Source; Bbc swahili

No comments

Powered by Blogger.