Header Ads

Anayoyafanya Jaji Warioba hata Mwalimu Nyerere Aliyafanya pia!

WAVURUMISHAO makombora dhidi ya Jaji Joseph Warioba wamekuwa wakitoa hoja kwamba mzee huyo muda wake wakuzungumzia suala la katiba mpya ulishamalizika kwa minajili kuwa Tume yake ya kukusanya maoni ya Katiba mpya ilishavunjwa.

Kelele zimepigwa katika bunge maalum la katiba, mtaani wanasema “mzee pumzika muda wako umekwisha” hawataki tena atumie uhuru wake wa kikatiba kuzungumzia mambo ambayo yeye anaona hayajaenda sawa, wao wazungumze yeye anyamaze, au sasa hivi kuna sheria inasema ni wakati wa Chama fulani tu peke yake kujimwaya mwaya uwanjani na kuipamba katiba pendekezwa.

Nafurahi wanaomkosoa Mzee Warioba wamekuwa wakijinadi kuwa wao ni wafuasi wazuri sana wa hayati Mwalim Julius Nyerere, wamekuwa wakitusihi kila uchao tuige yale mazuri aliolifanyia taifa hili, wanatwambia tutunze amani, tuache ubaguzi na mbwembwe za kila aina.

Wanatwambia Mwalimu Nyerere alikuwa mstari wa mbele kulipigania taifa hili, alikuwa mzalendo, aliyapigania mataifa mengine ya Afrika, mfano wa Afrika Kusini, Msumbiji nakadhalika, kuhakikisha yanapata uhuru wao, hata Rais Kikwete kuhutubia mazishi ya Mandela na akaeleweka vema ni kutokana na jithada za Mwalimu alizozifanya huko nyuma katika taifa hilo.

Wakati wakimuona Mwalimu Nyerere kama mzalendo huku wakitutaka tumuige mzee huyo, kwa bahati mbaya wale wanaitika wito wao wakututaka tufanye hivyo wanawaona kama nuksi sasa, wanawatwisha majina ya kila aina, wavunjaamani, wazushi, ni shidaaa na mengineyo.

Soma zaidi hapa; Mpekuzi

No comments

Powered by Blogger.