Header Ads

Unahitaji kujua umebakiwa na siku ngapi za kuishi duniani? Ipo app ya simu itakayokupa jibu

Ukuaji wa teknolojia unazalisha stori mpya kila siku ila leo huenda ukashtuka; unajua simu yako
inaweza kukwambia siku yako ya kufa?.

‘Macabre iPhone App’ ni application ambayo unaweza kuiweka kwenye simu yako na jukumu ambalo utakuwa nalo ni kuweka ratiba zako zote za siku nzima, application hiyo inapiga hesabu halafu inakupa majibu siku zako ngapi zimesalia
kuishi duniani.

Kali zaidi ni kwamba majibu utakayopewa ya idadi ya miaka, miezi, wiki, siku na saa itakuwa
inaonekana kwenye screen lock, kwa hiyo kila unapotoa lock ya kwenye screen itakuwa inaonekana hapo juu.

Majukumu yako ya siku ndiyo yataakayoamua siku ngapi utaishi.

Application hiyo inapatikana kwa simu za Apple zinazotumia iOS na Windows 8.
Unadhani uko tayari kuitumia application hii?

No comments

Powered by Blogger.