ARSENAL NI VIBONDE WA 'KUPIKA NA KUPAKUA' KWA MAN UNITED, MECHI 11 ZILIZOPITA WAMESHNDA MOJA TU!
MECHI kati ya Arsenal dhidi ya Manchester United wakati wote imekuwa moja ya michezo ya kusisimua katika historia ya Ligi Kuu ya England – lakini The Gunners wameshinda mechi moja tu kati ya 11 zilizopita baina ya klabu hizo.
Louis van Gaal atasafiri na kikosi chake chenye majeruhi kibao hadi Uwanja wa Emirates Jumamosi mchana akitambua kwamba timu
yake imekuwa na historia nzuri siku za karibuni dhidi ya wapinzani wake hao.
Licha ya kuboronga msimu uliopita, lakini bado United ilijimudu kuichapa Arsenal 1-0 Uwanja
wa Old Trafford na kutoka nayo sare ya bila kufungana katika mchezo mwingine Kaskazini mwa London.
Wakati kocha Sir Alex Ferguson akiwa katika msimu wake wa mwisho Old Trafford, mabao ya
Robin van Persie na Patrice Evra yaliipa United ushindi wa 2-1 nyumbani wakati Van Persie pia
alifunga tena dhidi ya Arsenal aliporejea Emirates baadaye msimu huo kusawazisha baada ya Theo Walcott kuanza kufunga na
kufanya sare ya 1-1.
Ushindi wa mwisho wa Arsenal katika Ligi Kuu ya England dhidi ya United ulikuwa Mei mwaka 2011 wakati Aaron Ramsey alipofunga bao pekee katika ushindi wa 1-0 nyumbani.
Kutoka kwenye kikosi cha Arsenal wakati huo, wachezaji watano bado wapo klabuni, akiwemo kipa Wojciech Szczesny, Laurent Koscielny, Walcott, Ramsey na Jack Wilshere.
Lakini ikiwa Wenger anatafuta ahueni anahitaji kutazama juu ya rekodi ya ugenini ya United, bado hawajashinda mechi yoyote ugenini msimu huu na hawajachukua pointi tatu katika mechi zao za ugenini tangu Aprili 5, mwaka huu walipoifunga Newcastle 4-0.
Misimu iliyopita, mechi kati ya Arsenal vs Manchester United ilikuwa ya kuamua bingwa, lakini mwaka huu inaonekana kama ni mechi ya kuwania nafasi ya nne na ya mwisho ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Lakini kikubwa zaidi, The Gunners wanatarajiwa kufuta uteja wao kwa United.
Matokeo ya Mechi Mbali mbali kati ya Man u vs Arsenal;
2, 2014 Arsenal 0-0 Man Utd
0, 2013 Man Utd 1-0 Arsenal
, 2013 Arsenal 1-1 Man Utd
, 2012 Man Utd 2-1 Arsenal
2, 2012 Arsenal 1-2 Man Utd
8, 2011 Man Utd 8-2 Arsenal
, 2011 Arsenal 1-0 Man Utd
3, 2010 Man Utd 1-0 Arsenal
1, 2010 Arsenal 1-3 Man Utd
9, 2009 Man Utd 2-1 Arsenal
6, 2009Man Utd 0-0 Arsenal
Post a Comment