Sumaye: Sababu yangu najitosa kusaka urais
Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, ametaja sababu tatu za kuwania urais katika uchaguzi
mkuu wa mwakani, akieleza kuwa mojawapo ni kukuza uchumi unaogusa maisha ya Watanzania
wengi.
Akizungumza na vyombo vya habari wiki iliyopita katika mahojiano maalum nyumbani kwake Kiluvya, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, Sumaye (64), alisema suala la pili linalomsukuma kuwania nafasi
ya kuwa mkuu wa nchi ni vita dhidi ya rushwa, ufisadi na dawa za kulevya.
Alitaja kipaumbele chake cha tatu kuwa ni kuundaserikali inayowajibika kwa umma, kwa kuweka watu ambao wataweka mbele maslahi ya umma badala ya maslahi binafsi.
“Mimi nimeshasema kwamba muda ukifika nitajitosa tu kwa sababu Watanzania wengi wananiambia nijitose na sina sababu ya
kuwakatalia. Muda ukifika na mimi nitatangaza… kwamba sasa na mimi nipo rasmi kwenye kinyang’anyiro hicho,” alisema Sumaye.
Sumaye ambaye anashikilia rekodi ya kukalia kiti cha Waziri Mkuu kwa miaka 10 mfululizo zaidi ya wengine wote walioshikilia nafasi hiyo chini ya uongozi wa awamu ya tatu ya Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, alisema iwapo atafanikiwa kuteuliwa na CCM kushika wadhifa huo, atakuwa na vipaumbele vichache ili aweze kuvisimamia kwa ukamilifu.
Bofya hapa kusoma zaidi; NIPASHE
Post a Comment