Header Ads

MAN UNITED YAIZIMA ARSENAL, YAICHAPA 2-1 - EMIRATES

MANCHESTER United imeendeleza ubabe dhidi ya Arenal, baada ya usiku huu kuichapa mabao 2-1 Uwanja wa Emirates katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.

United walipata bao la kwanza dakika ya 56, baada ya beki Kieran Gibbs kumfunga mwenyewe kipa wake, Wojciech Szczesny katika harakati za kuokoa krosi ya Antonio Valencia, kabla ya Nahodha Wayne Rooney kufunga la pili dakika ya 85 akimalizia pasi ya Angel di Maria. Olivier Giroud aliifungia Arsenal
la kufutia machozi dakika ya 90.

Beki wa United, Luke Shaw alitolewa nje dakika ya 16 baada ya kuumia kifundo cha mguu, wakati kiungo wa Arsenal, Jack Wilshere alinusurika kupewa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Marouane Fellaini.

Lakini kiungo huyo wa England alitolewa nje dakika ya 55 baada ya kuumia pia. Kipa Szczesny pia alitolewa uwanjani baada ya kuumia.

Kikosi cha Arsenal kilikuwa; Szczesny/Martinez dk59, Chambers, Mertesacker, Monreal, Gibbs, Ramsey/Giroud dk77, Arteta, Wilshere/Cazorla dk55, Oxlade-Chamberlain, Welbeck na Sanchez Manchester United; De Gea, Smalling, McNair, Blackett, Valencia, Carrick, Fellaini, Di Maria, Shaw/Young dk16/Fletcher dk89, Rooney na Van Persie/James Wilson dk75.

No comments

Powered by Blogger.