Header Ads

Utawala kurejeshwa kwa Raia - Burkina Faso

Muundo wa Serikali ya mpito nchini Burkina Faso umeridhiwa baada ya mazungumzo kati ya Viongozi wa siasa, Jeshi na Viongozi wa Asasi za kiraia.

Msemaji wa mazungumzo hayo mjini Ouagadougou amesema kuwa makubaliano hayo yamefikiwa kwa pamoja na Viongozi hao.

Uongozi wa mpito wa sasa umedhamiria kurudisha nchi kwa utawala wa kiraia na kujiandaa na
uchaguzi mwakani.

Jeshi lilichukua madaraka baada ya Rais Blaise Compaore kushurutishwa kujiuzulu tarehe 31
baada ya maandamano makubwa.

Luteni kanali Isaac Zida alijitangaza kuwa Kiongozi wa Burkina Faso tarehe 1 mwezi Novemba baada
ya Rais Compaore kutorokea nchini Ivory Coast baada ya kuwa madarakani kwa miaka 27.

Source; BBC SWAHILI

No comments

Powered by Blogger.