Header Ads

MSUVA ‘AZIMWAGA MATE’ SIMBA NA AZAM

WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva anazivutia Azam FC na Simba SC, lakini bahati nzuri, au mbaya yuko katika mwaka wa kwanza wa Mkataba wake mpya wa miaka miwili na klabu yake, Yanga SC.

Simba na Azam FC, zote zilijaribu kutaka kumsajili kijana huyo mwishoni mwa msimu uliopita, lakini zikachelewa na kukuta
amekwishasaini Mkataba mpya Jangwani.

Kwa sasa inaaminika Msuva ndiye winga bora zaidi Tanzania, ingawa ameshindwa kumshawishi kocha wa Taifa Stars, Mholanzi
Mart Nooij kumpa nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

Msuva amekuwa mkali kwa misimu takriban miwili akitamba Yanga SC, lakini hata mbele ya kocha aliyetangulia Taifa Stars, Mdenmark, Kim Poulsen hakuwahi kuwa na nafasi katika kikosi cha kwanza.

Tangu ajiunge na Yanga SC akitokea Moro United mwaka 2012, Msuva tayari amekwishaichezea timu hiyo mechi 72 na kuifungia mabao 17.

Tayari amempiku kwa mbali, mshambuliaji Said Bahanuzi waliyesajiliwa pamoja, akitokea
Mtibwa Sugar, ambaye hadi sasa ana mechi 48 na mabao 15, matatu kati ya hayo ya penalti.

Bahanuzi alikuwa ana mwanzo mzuri Yanga SC akitoa mchango mkubwa kwa timu hiyo kutwaa
ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame- tena akiibuka mfungaji bora katika
michuano hiyo iliyofanyika Dar es Salaam.

Lakini makali yake yaliyeyuka ndani ya msimu wake huo huo wa kwanza- baada ya kusajiliwa mshambuliaji Mrundi, Didier Kavumbangu, aliyecheza misimu miwili Jangwani.

Kavumbangu aliondoka Yanga SC mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kuichezea timu
hiyo jumla ya mechi 63 na kuifungia mabao 31, moja la penalti. Lakini ujio wa Mbrazil Genilson
Santana Santos ‘Jaja’ umezidi kumuweka katika wakati mgumu Bahanuzi na tayari kuna dalili za kutosha anaweza kuonyeshwa mlango wa kutokea baada ya msimu huu.

Source; BIN ZUBEIRY

No comments

Powered by Blogger.