Header Ads

Risasi zatumika Kuwatawanya WEZI wa mafuta, Waliovamila Lori lililopata Ajali - Tabata Kisiwani

Jeshi la Polisi limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi waliokuwa wakichota
mafuta yaliyomwagika kutoka kwenye lori la mafuta aina ya scania lililopata ajali.

Usiku wa kuamkia jana mida ya saa tatu, baada ya lori hilo lililobeba shehena ya mafuta ya petroli, kushindwa kupanda mlima, kuserereka kisha kupinduka, eneo la Tabata Kisiwani kwa Mama Pindapinda.

Baada ya ajali hiyo, mafuta yalianza kumwagika na kuwavutia wakazi wa jirani na eneo hilo waliobeba vyombo mbalimbali yakiwamo
mabeseni na ndoo za maji ili kuchota nishati hiyo, Mjumbe wa Mtaa Bonde la Mchicha, Tabata
Kisiwani, Mama Pindapinda alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

"Nilipiga simu polisi kuwataarifu
na walifika, lakini baada ya gari hilo kuondolewa eneo la tukio, polisi nao waliondoka usiku wa saa 8 ".Alisema Mama Pinda pinda.

Hadi kufikia saa 3 asubuhi, waendesha bodaboda waliendelea kumiminika eneo hilo, wengi wakiwa
na chupa kubwa za maji ya uhai, madumu ya lita 20 na yenye ujazo wa lita tano wakisomba mafuta
hayo.

Hata hivyo, tafrija hiyo ya mafuta haikudumu kwa muda mrefu, kwani ilipofika saa tano asubuhi,
kundi la Jeshi la Polisi na Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia(FFU), walifika eneo hilo na kuanza
kuwatawanya wakazi hao kwa risasi, ambapo walianza kukimbia huku na kule.

Source; Mpekuzi

No comments

Powered by Blogger.