Header Ads

Manchester United Wapata Kipigo dhidi ya Man City

Ligi kuu ya soka nchini England imeendelea hii leo kwa michezo miwili iliyopigwa huko jijini Manchester na jijini Birmingham.

Katika mchezo wa kwanza Mabingwa watetezi wa ligi hiyo Manchester City waliwafunga mahasimu wao wa jadi Manchester United kwa bao moja bila katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Etihad .

Bao pekee lililoamua mchezo huo lilifungwa na mshambuliaji raia wa Argentina Sergio Kun Aguerro ambaye alimalizia pasi ya Gael Clichy.

United katika mchezo huo ilimaliza ikiwa pungufu baada ya mlinzi Chris Smalling kuonyeshwa kadi nyekundu mapema kwenye
kipindi cha kwanza .

Matatizo ya United hayakuishia hapo kwani baadaye mlinzi wa kimataifa wa Argentina Marco Rojo alilazimika kutolewa nje baada ya kuumia bega lake.

Huu ni ushindi wa nne mfululizo ambao City inaupata mbele ya United huku Sergio Aguerro akiendelea kuwaumiza mashetani wekundu akiwa amefunga mabao matano kwenye michezo sita dhidi ya United .

No comments

Powered by Blogger.