Header Ads

DIAMOND, ZARI MAHABA MAZITO

Siku chache baada ya kumwagwa na Wema Isaac Sepetu ‘ Beautful Onyinye’ , Mbongo Fleva , Nasibu Abdul ‘ Diamond Platnumz ’ amenaswa kwenye mahaba mazito na msanii, mtangazaji, mjasiriamali, tajiri na mrembo mkali kuliko wote Afrika Mashariki, Zarinah Hassan a . k . a Zari au Boss Lady.

Kwa mujibu wa chanzo makini, mastaa hao walipokutana kwenye ndege waliungana na kupiga picha za pamoja kisha safari yao ya
mahaba niue ikaanzia hapo.

UWANJA WA NDEGE
Chanzo hicho kilimwaga ‘ ubuyu’ kwamba, wawili hao walipotua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Diamond alionekana akiwa ‘ veri klozi ’ na Zari kiasi cha kuibua minong ’ oni uwanjani hapo kwa namna walivyoonekana wamependezeana.

Chanzo hicho ambacho ni mtu wa karibu wa Diamond au Dangote, kilizidi kuvujisha kwamba, ilipofika usiku , wawili hao waliamua
kuhama kwenye hoteli hiyo kwa madai kwamba walikuwa wameshtukiwa na watu wengi hivyo walihofia kunaswa, Ilisemekana kwamba walihamia hoteli nyingine ambayo nayo ipo pembezoni mwa ufukwe huo.

Bofya hapa kusoma zaidi; GPL

No comments

Powered by Blogger.