Header Ads

Raia Mwingine wa Marekani akatwa shingo na IS

Kanda moja ya video iliowekwa mtandaoni inaonyesha mauaji ya mtu wa kutoa huduma za
misaada raia wa Marekani Abdul Rahman Kassig ambaye alikuwa anajulikana kama Peter Kassig
kabla ya kutekwa nyara na wanamgambo wa Islamic State nchini Syria mwaka uliopita.

Video hiyo inamuonyesha mawanamume mmoja anayeonekana kuwa mwanachama wa Islamic State akiwa na kisu mkononi na maandishi yanayosema
kuwa Peter Kassig ameuawa.

Kanda hiyo pia ina picha za watu kadha waliouawa ambao wanasemekana kuwa wanajeshi wa Syria waliokuwa wametekwa nyara.

Marekani imesema kuwa inafanya juhudi za kubaini chimbuko la kanda hiyo.

Bwana Kassig ambaye anajulikana kama Peter alitekwa nyara mwaka uliopita.

Mnamo mwezi Octoba kanda nyengine ya video ya kifo cha mfanyikazi mwengine wa misaada kutoka Uingereza Alan Henning iliisha huku Kassig akitishiwa.

Source; BBC SWAHILI

No comments

Powered by Blogger.