Header Ads

(ESCROW) WATIKISA BUNGE LA TANZANIA, WABUNGE WA CCM NA UPINZANIA WACHACHAMAA

SAKATA LA UCHOTAJI WA FEDHA
AKAUNTI YA TEGETA (ESCROW)
WATIKISA BUNGE LA TANZANIA,
WABUNGE WA CCM NA
UPINZANIA WACHACHAMAA

WABUNGE jana waliungana bila kujali vyama vyao, kutetea kuwasilishwa bungeni na kujadiliwa kwa ripoti ya sakata la uchotaji fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow baada ya kuwapo kwa taarifa kuwa Mahakama imezuia.

Katika kile kilichoonekana kuwa wabunge wanataka mbivu na mbichi za sakata hilo ziwekwe hadharani, walisema hatua yoyote ya kuzuia suala hilo lisijadiliwe, inaweza kulivuruga Taifa na wao
kulaumiwa.

Hata hivyo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alitoa angalizo kuwa ni vyema kuwapo kwa utulivu na kila mhimili kusimamia mamlaka yake, na busara kutumika.

Bunge liliingia katika mjadala baada ya Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi), kuomba ufafanuzi kutokana na kauli ya Waziri Mkuu wakati wa kipindi cha Maswali ya Papo kwa Hapo.

Akijibu swali la Mbunge wa Mbozi Magharibi, David Silinde (Chadema), Waziri Mkuu Pinda alisema yeye kama Mwanasheria ingawa si Mwanasheria Mkuu, kuna kesi zaidi ya 10 mahakamani kuhusu hilo, hivyo si vyema kuanza mjadala utakaotibua suala hilo.

Alisema hiyo si mara ya kwanza kwa Bunge kutoshughulika na suala linaloendelea mahakamani.

Kauli hiyo ndiyo iliyomsimamisha Kafulila na wabunge wengine wawili, Esther Bulaya (Viti Maalumu – CCM) na Moses Machali (Kasulu Mjini – NCCR- Mageuzi), huku Kafulila akitaka uhakika wa kauli ya Waziri Mkuu kama ripoti hiyo itapelekwa bungeni kujadiliwa au la.

    Soma zaid>>>>

No comments

Powered by Blogger.