Header Ads

VYAMA VITANO VYA SIASA VISIVYO NA WABUNGE VYAOMBA SAKATA LA IPTL LIMALIZWE

MAKATIBU wakuu wa vyama vitano vya kisiasa visivyo na wabunge bungenivwameomba suala la utata wa ufisadi zaidi ya sh.bilioni 300 zilizowekwa katika akaunti ya Tegeta Escrow zilizokuwa Benki
Kuu ya Tanzania (BoT) limalizwe ili
kuendelea kwa mambo mengine ya kitaifa.

Katika hatua nyingine makatibu hao
wamepinga hatua ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (Takukuru) kukabidhi ripoti ya uchunguzi kwa Waziri Mkuu na kudai ipelekwe kwa Mkurugenzi
wa Mashtaka nchini (DDP) mwenye uwezo wa kuchukua hatua za kisheria.

Makatibu hao ni kutoka Chama cha Kijamii (CCK), Sauti ya Umma (SAU), Union For Multiparty Democracy (UMD), Alliance Farmaers Party na Demokrasia Makini (DM) ambavyo vimetoa tamko hilo Dar es
Salaam leo wakati wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu sakata hilo linaloendelea bungeni mjini Dodoma.

Tamko la makatibu hao limekuja siku moja tu baada ya kuwepo taarifa kuwa Waziri Mkuu, Pinda atakabidhi kwa Spika wa
Bunge, Anne Makinda ripoti ya ukaguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali (CAG) kuhusu akaunti ya Tegeta
Escrow kufuatia madai ya uchotwaji wa Dola za Marekani milioni 200 (Sh. bilioni 320).

Makatibu wakuu wa vyama hivyo,Renatus Muabhi (CCK), ,Ali Kaniki (SAU), Rashid Rai (AFP),Dominick Lyamchai (Demokrasia Makini)na Kibaya Kiahira (UMD) walisema
Takukuru kupeleka ripoti ya uchunguzi wa suala hilo bungeni siyo sahihi kwasababu
ina utaratibu wake wa kufanya kazi kwa mujibu wa sheria.

Kiutaratibu Takukuru wakikamilisha
uchunguzi wa jambo lolote inatakiwa kisheria kupeleka ripoti hiyo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka wa Serikali (DPP) na baada ya DPP kuipitia atatoa maoni
yake ya kisheria kama kuna umuhimu wa kufungua mashtaka,”alisema Ali Kaniki
Katibu Mkuu wa chama cha SAU.

Bofya hapa kusoma zaid; Michuzi blog

No comments

Powered by Blogger.