Header Ads

RONALDO AWEKA REKODI NYINGINE, AFUNGA BAO URENO IKICHINJA ARMERIA - ULAYA


URENO imeilaza bao 1-0 Armenia mjini Faro usiku wa kuamkia leo katika mchezo wa Kundi
Ia kufuzu Kombe la Mataifa ya Ulaya, maarufu kama Euro 2016.

Shukrani zimuendee Mwanasoka Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 71 kuipatia pointi muhimu nchi
yake katika mbio hizo- ambalo linakuwa bao lake la 23 kwenye mechi za kufuzu za Euro na
kuweka rekodi ya mchezaji aliyefunga mabao
mengi zaidi kwenye michuano hiyo.

Ushindi huo, unaifanya Ureno ifikishe pointi sita baada ya kucheza mechi tatu na kupanda nafasi ya pili kwenye kundi hilo, nyuma ya Denmark wanaoongoza kwa pointi zao saba za mechi nne.

Albania ina pointi nne za mechi tatu, wakati Serbia na Armenia zina pointi moja kila moja baada ya kucheza mechi tatu.

Aidha, kwa mshambuliaji huyo wa klabu bingwa Ulaya, Real Madrid- Ronaldo kutokana na kufunga bao hilo pekee jana, anakuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi kwenye michuano hiyo ya Ulaya.

Kikosi cha Ureno kilikuwa; Patricio, Bosingwa, Pepe, Carvalho, Guerreiro, Nani/Carvalho, Moutinho, Tiago, Ronaldo, Postiga/Eder na Danny/Quaresma.

Armenia: Berezovsky, Hovhannisyan, Haroyan,
Arzumanyan, Taron Voskanyan, Hayrapetyan, Mkrtchyan/Pizzelli, Mkhitaryan, Yedigaryan/
Sarkisov, Ghazaryan/Manucharyan na Movsisyan.

Hata hivyo, sasa ndiye mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi kwenye historia ya michuano ya Ulaya kufuatia bao lake la dakika ya 71 dhidi ya Armenia jana.
Akiwa amefikisha mabao 23 kwenye mechi za kufuzu na Fainali pia za Euro, Nahodha huyo wa Ureno anampiku Jon Dahl Tomasson wa
Denmark, ambaye amestaafu soka ya kimataifa mwaka 2010.

No comments

Powered by Blogger.