Header Ads

DIWANI WA CCM AOMBA KUMTWANGA NGUMI DIWANI WA CHADEMA - KAHAMA

KIKAO cha kawaida cha baraza la madiwani wa halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama Mkoani
Shinyanga Juzi lililazimika kusimama kwa muda baada ya kutokea ugomvi wa kurushiana maneno na Kejeri kwa baadhi ya Madiwani wa halmashauri
hiyo huku wengine wakiomba dakika kumi kupigana ndani ya kikao hicho.

Hali hiyo ilijitokeza wakati Diwani wa Kata ya Idahina Sospeter Bunanda (CHADEMA) Kusimama
na kutoa ushauri kwamba mabaraza ya ardhi ya Kata wapewe semina ya uendeshaji wa mabaraza hayo kuliko kutumia vipeperushi walivyopewa na Mwanasheria katika halmashauri hiyo ili
kuwajengea uwezo mkubwa wa kutatua migogoro
ya ardhi katika kata zao.

Kufuatia hali hiyo Diwani wa kata ya Sabasabini Emmanuel Makashi (CCM) alisimama na kumwomba mwenyekiti wa Halmashauri hiyo
Juma Kimisha, Kutupilia mbali maombi hayo kwani kusema hivyo ni kumfundisha mwanasheria wa ambaye tayari anataaluma yake huku akisema alikasilishwa na kitendo cha diwani huyo kuwa anaingilia ya wachangiaji wengine wakati hajaruhusiwa na mwenyekiti.

Bunanda alisimama tena na kuomba mwongozo kwa mwanasheria kwamba “Ni halali serikali wa kuendesha vikao vya vyake kwa kutumia vipeperushi”? na ndipo vurugu ya maneneo ilitawala ndani ya ukumbi huo ambapo Diwani Makashi alimtaka Mwenyekiti wa halamshauri kumpatia Dakika Kumi ili ampige makonde diwani wa Kata ya Idahina, Bunanda akimtuhumu kwamba anapinga mabaraza hayo.

“Mheshimiwa Mwenyekiti naomba uniruhusu dakika kumi tu tupigane na huyu jamaa, na sitafungwa jela wala kesi yoyote san asana zitafungwa hela tu, niruhusu Mwenyekiti maana anadakikadakia tu muda wa watu wengine kwa kuchangia hoja ambazo ni za kupinga, na asituletee uchadema hapa” Alisema kwa jazba
Makashi.

Kufuatia hali hiyo ambayo ilidumu kwa takribani Dakika tano, Mwenyekiti wa kamati ya Maadili Kulwa Shoto aliingilia kati na kukemea kitendo hicho na kuwaomba madiwani hao kutotumia kauli kali ambazo zinaweza kusababisha vurugu.

Aidha, Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Juma Kimisha aliwataka madiwani kuzitambua sheria, kanuni na miongozo ya baraza la madiwani pamoja na kuwa wavumilivu juu ya kauli na maoni yaw engine.

Hata hivyo hali ilirejea kawaida na kikao hicho kuendelea kama kawaida ambapo pamoja na mambo mengine Kimisha aliwataka madiwani kutumia muda wao kuhamasisha maedeleo katika kata zao hususani kutekeleza agizo la Rais Jakaya Kikwete la ujenzi wa maabara tatu kila
Shule ya Sekondari.

Source; Kijukuu cha Bibi k-blog

No comments

Powered by Blogger.