Header Ads

REAL MADRID YAIZIMA 1-0  LIVERPOOL LIGI MABINGWA ULAYA

BAO pekee la Karim Benzema usiku huu limeipa ushindi wa 1-0 Real Madrid katika mchezo wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Liverpool, Uwanja wa Bernabeu, Madrid.

Mfaransa huyo alifunga bao hilo dakika ya 27 katika mchezo ambao, kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers aliwapumzisha wachezaji
wake saba wa kikosi cha kwanza, akiwemo Nahodha Steven Gerrard na mshambuliaji
Mario Balotelli Gerrard na Raheem Sterling walitokea benchi
dakika ya 69 kwenye mchezo huo, ambao Mwanasoka Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo alipoteza nafasi kadhaa za kufunga.

Ushindi huo, unaifanya Real itimize pointi 12 baada ya kucheza mechi nne na kushinda zote, ikifuatiwa na FC Basel yenye pointi sita, Liverpool tatu sawa na Ludogorets Razgrad, zote pia zimecheza mechi nne kila moja.

Mchezo mwingine wa kundi hilo usiku huu, FC Basel imeshinda 4-0 dhidi ya Ludogorets Razgrad, mabao ya Breel Embolo dakika ya 34, Derlis Gonzalez dakika ya 41, Shkelzen Gashi dakika ya 59 na Marek Suchy dakika ya
65.

Kikosi cha Real Madrid kilikuwa: Casillas, Arbeloa/Nacho dk83, Varane, Ramos, Marcelo, Modric, Kroos, Isco, Rodriguez/Bale dk62, Ronaldo na Benzema/Hernandez dk87.

Liverpool; Mignolet, Manquillo, Toure, Skrtel, Moreno, Can/Coutinho dk75, Lucas/Gerrard dk69, Lallana, Allen, Markovic/Sterling dk69

No comments

Powered by Blogger.