Header Ads

MTOTO WA RAIS KIKWETE AKANUSHA KUMILIKI KAMUNI YA SIMBA TRUST

Mtoto wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Miraji Kikwete usiku wa Nov 11 2014 ameeleza kuhusu uvumi uliosambazwa kwamba anamiliki kampuni ya Simba Trust
iliyopo Australia akishirikiana na dada yake.

Kufuatia tuhuma hizo Miraji alipost
maandishi akikanusha hiyo ishu akisisitiza kwa eleweke hivi ningekuwa napokea milioni
100 kwa siku wallahi ningeshukuru kwa mola ila siwezi kuchukua fedha kinyume na haki ninayo stahili.

"Katika jambo lililonishangaza ni hizi tuhuma za kuwa ninamiliki kampuni ya Simba trust ya Australia mimi na dada yangu Salama, naona sasas mmeishiwa hoja na
kuanza kuzusha mambo, sijawahi kufika Australia na sina kampuni ninayomiliki na dada yangu, lakushangaza kwanini PAP
wanilipe pesa bila sababu maalum’
‘Sina pesa nyingi kiasi hicho, kidogo
ninachokipata ni kwa jasho langu, sijawahi na sitodiriki kupokea pesa ambazo si haki yangu kupata." Alisema Miraraji.

Hata hivyo, amewabia waache kupandikiza chuki zisizo na ukweli wowote, atakaethibitisha basi na aonyeshe hilo kwa vielelezo na ushahidi, chuki hazijengi, kweli umeishiwa hoja na mambo ya msingi ya kujadili.

No comments

Powered by Blogger.