Header Ads

WAVUVI HARAMU WALIPUKIWA NA MABOMU WAPOTEZA MIKONO, MACHO - TANGA

Wakazi wawili wa kata ya Tangasisi
tarafa ya Pongwe wilayani Tanga
wamejeruhiwa vibaya viungo mbalimbali vya mwili kwa kulipukiwa na baruti wakati wakivua kwa kutumia dhana za uvuvi haramu kwenye kisiwa cha
Karange.

Tukio hilo limetokea mnamo Novemba 12 mwaka huu majira ya saa nane mchana katika kisiwa ambapo majeruhi hao wakiwa kwenye ngalawa yenye namba za usajili TTA 315 wakati wakijianda kutegesha baruti hizo ndipo zilipowalipukia.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga
Freisse Kashai amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataja majeruhi hao kuwa ni Hamis Omari ambaye amekatika mkono wa kulia na ameumia jicho la kulia,huku majeruhi mwingine Adamu Selemani amekatika mikoni yote miwili, pamoja na kupoteza macho yote mawili.

“Hali ya majeruhi wote wawili ambao wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya bombo ni mbaya hii inaonyesha ni kwa kiasi gani uvuvi haramu ulivyo na madhara makubwa kwa jamii pamoja na viumbe wa baharini “alisema Kamanda
Kashai.

Hata hivyo kamanda Kashai alitumia fursha hiyo kuwa taka wakazi wanaoishi maeneo ya bahari kutoa taarifa ya wavuvi wanaojihusisha na uvuvi haramu ili kuweza kuwachukulia hatua mapema kabla ya kutokea kwa madhara zaidi.

No comments

Powered by Blogger.