Header Ads

SUAREZ AIFUNGIA URUGUAY KATIKA SARE YA 3-3 NA COSTA RICA KABLA YA KUFA KWA PENALTI

MSHAMBULIAJI Luis Suarez ameisaidia Uruguay kupata sare ya 3-3 dhidi ya Costa Rica mjini Montevideo, lakini wenyeji
walifungwa kwa penalti 7-6 baada ya Johan Venegas kufunga bao la kusawazisha dakika za mwishoni.

Nyota huyo wa Barcelona alifunga mapema kipindi cha pili baada ya Alvaro Saborio kuwafungia wageni bao la kuongoza.

Bryan Ruiz akawafungia Costa Rica bao la pili ndani ya dakika ya moja baada ya Suarez kufunga, lakini mabao mawili ndani ya dakika tatu kutoka kwa Jose Gimenez na Edinson Cavani yaliisogeza Uruguay karibu na ushindi.

Suarez, ambaye alichaniwa kipande cha jezi, alifunga penalti ya kwanza ya Uruguay, lakini Celso Borges akakosa ya Costa Rica.

Baada ya kufunga penalti sita mfululizo, Arevalo Rios alipata nafasi ya kuipa ushindi Uruguay,
lakini mkwaju wake uliokolewa na kipa wa Real Madrid, Keylor Navas.

Huku timu hizo zikiwa zimefungana penalti 6-6, Guzman Costa Rica pia ilishinda 3-1 timu hizo zilipokutana katika mchezo wa Kundi D Kombe
la Dunia mjini Fortaleza.

No comments

Powered by Blogger.