Header Ads

PIGO MAN UNITED, MARCOS ROJO NJE MIEZI MITATU BAADA YA KUUMIA BEGA

BEKI wa Manchester United, Marcos Rojo anatarajiwa kuwa nje hadi miezi mitatu baada ya kuumia beta katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana dhidi ya Manchester City.

Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Etihad na Manchester United kuchapwa 1-0, beki huyo alitolewa nje kwa machela dakika ya 56 baada ya kuumia wakati aliokoa kwa kuutelezea mpira.

Hali ya Rojo si nzuri na mlinzi huyo wa kimataifa wa Argentine atakosekana kwa angalau wiki sita.

No comments

Powered by Blogger.