PICHA: MBOWE ATINGA MAKAO MAKUU YA POLISI KUHOJIWA, WANACHAMA WAZUA TIMBILI
- MNYIKA, WANASHERIA WAZUIWA KUINGIA NDANI
- WANAHABARI WAKIMBIZWA NA MBWA, WAUMIA, WAMWAGA MACHOZI
MAMIA
ya watu wamejitokeza leo kumsindikiza Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, baada ya kuhitajiwa
kufika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi nchini, jijini Dar es Salaam
kuhusiana na kauli yake aliyotoa majuzi juu ya kuitisha maandamano nchi
nzima kupinga kuendelea kwa Bunge Maalum la Katiba.
Kilichofuata
ni polisi kuamuru watu wote waondoke eneo hilo kwa umbali wa mita 200
ambapo walikimbizwa na mbwa wa polisi na kusababisha wengi wao waumie na
kupoteza vitu vyao mbalimbali, hususani wanahabari ambao baadhi yao
waliumia na kupoteza zana zao za kazi.
SOURCE: GLOBAL
Post a Comment