FAHAMU MAKOSA 9, AMBAYO WENGI WETU TUNAYAFANYA TUNAPOTOKA MTOKO NA MTU WA JINSIA TOFAUTI SIKU ZA MWANZONI
Iwe ni mara yako ya kwanza,
au umezoea kutoka na mtu wa
jinsia tofauti lazima kuna vitu uzingatie ili usiharibu ladha na maudhui ya
mtoko wako.
Kwani ni ukweli ulio wazi kuwa
mpaka umekubali kupata mtoko na mtu wa jinsia tofauti maana yake unafurahia
uwepo
wake karibu yako.
Na pengine ushaanza fikiria
mipango ya baadaye ukiwa naye.
Lakini kuna makosa ambayo
tunayafanya wengi wetu siku ya kwanza unapotoka na mtu wa jinsia tofauti.
Pitia vipengele vifuatavyo
ugundue unafanya wapi makosa na uyaepuke.
1.USIMZUNGUMZIE MTU WAKO ALIYEPITA
Hili ndio kosa kubwa la kwanza
ambalo wengi wanalifanya wanapokuwa katika mtoko na mtu mwengine wa jinsia
tofauti.
Tambua wazi si kwamba
utamuonyesha kuwa una hisia na watu unaowahi kuwa nao,
lakini ujue unamuudhi
mtu uliyetoka naye.
Kuleta suala la mtu mwengine
aliyepita wakati uko na mwengine halina maana yoyote kama umekosa la kuongea
heri unyamaze hadi uulizwe.
2.USIZUNGUMZIE
NGONO
Kabla hujajua kama unayetoka
naye anapendelea mazungumzo ya aina gani,
usikurupuke kuzungumzia habari
hizo kana kwamba wewe ni mtaalamu sana ukidhani utamvutie uliyetoka naye.
Kama uliyetoka naye ana
malengo ya mbali utamfanya afikirie mara mbili kama utamfaa siku za mbele.
3.USIJIZUNGUMZIE
WEWE KILA WAKATI
Kujizungumzia wewe kila wakati
itamuonyesha uliyetoka naye kuwa una ubinafsi ndani yako.
Kila mtu angependa kupata
nafasi ya kujielezea mbele ya mwenzake lakini kama wewe unamkatisha na
kujizungumzia wewe tu utamtisha.
Ukionyesha unampa nafasi ya
kumsikiliza anachoongea yeye utamfanya aone wewe ni msikivu.
Na ukiwa msikivu kwa mwenzako
utapata nafasi ya kumtambua uliyetoka naye anapendelea mazungumzo ya aina gani.
4.IJUE HISTORIA
YAKE
Tafuta taarifa za mtu
unayetaka kutoka naye kabla haujafanya hivyo,
kwasababu wengine wana tabia
ya kurudia matukio mabaya waliyoyafanya siku za nyuma.
Ukijichanganya kutoka na mtu
bila kujua ana tabia gani anapofanya mtoko na mtu wa jinsia tofauti usije
ukakumbana na balaa.
Wengi walipatwa na mabaya kwa
kutojua historia ya wanaotoka nao na baadaye kujutia.
5.USITUMIE LUGHA
CHAFU
Hata kama ni kawaida yako
kuzungumza kwa
lugha chafu,
unapotoka na mtu kwa mara ya
kwanza jitahidi kuficha mizuka yako.
Kutumia lugha chafu kwa
kudhani utamuonyesha uliyetoka naye kuwa unajiamini na umuogopi ni kujiongopea.
6.KUVAA HOVYO
Tabia ya kumchukulia poa
unayetoka naye na kuvaa hovyo ili ujionyeshe kuwa unaamua unalotaka,
unaharibu taswira yako kwake.
Kwani wengi huona kama
umeshindwa kumuonyesha kumuheshimu siku ya kwanza au kabla hamjawa pamoja
inawezekana ukamuonyesha dharau zaidi utakapokuwa naye.
7.USIBEBE ZAWADI
ZA GHARAMA
Kumbuka huo ni mtoko tu na sio
sherehe.
Unapobeba zawadi za gharama
kubwa kwa mwenzako si kwamba utamfurahisha lakini ndani yake utamfanya akuone
kuwa upendo wako pia unajengwa zaidi na vitu vya gharama.
8.USISHAMBULIE
WENGINE
Ukiwa umetoka na mtu usianze
kumzungumzia vibaya mtu au watu wengine,
kwani utamuonyesha wazi kuwa
ipo siku na yeye itakuwa zamu yake.
9.USINYWE MPAKA
UKALEWA
Hata kama ulikuwa na kiu kubwa
ya kunywa pombe angalia usivuke kiwango mpaka ukalewa na usijielewe.
Tabia hii itamuonyesha ishara
mbaya juu yako.
UFANYE MTOKO WAKO
KUWA WA KAWAIDA,
MSAFI,
KUFURAHISHA,
NA WAKUKUMBUKWA.
ANZA SASA KUWA
MAKINI UNAPOKUWA UMETOKA NA MTU WA JINSIA TOFAUTI ILI USIHARIBU SIKU YAKO YA
KWANZA YA MTOKO NA KUMPOTEZA MTU AMBAYE UNGETAMANI AWE KARIBU YAKO.
Post a Comment