MKE AWAMWAGIIA MAJI YA MOTO MUME NA MWANAE
Ni hali ya kusikitisha na kustaajabu kwa jamii baada ya Tunu Kimaro kummwagia maji ya moto mumewe, William Mushi (32), mkazi wa Mabibo jijini Dar es Salaam pamoja na mtoto wake mchanga.
Tukio hilo la kikatili lilitokea Agosti 15, mwaka huu nyumbani kwake Mabibo jijini
Dar es Salaam na lilishangaza majirani kutokana na Tunu kudaiwa
kuchukuwa maji ya moto yaliyokuwa yanachemka na kuwamwagia bila huruma.
CHANZO NI MTOTO
Akisumulia mkasa huo Mushi alikuwa na haya ya kusema:
“Mke
wangu anaitwa Tunu Kimaro ana miaka 23. Alinimwagia maji ya moto baada
ya kumkuta mwanangu wa miezi saba hali yake ya kiafya ikiwa siyo nzuri,
nilipokuwa naondoka asubuhi nilimuagiza ampeleke hospitali.
Mtoto mchanga wa Bw.William Mushi aliyeunguzwa pia na maji ya moto.
“Baada ya kufika nyumbani na kumkuta mwanagu Ivan amenyong’onyea, nilipomuuliza mke wangu sababu za kutompeleka hospitali alinijibu majibu ya kijeuri kama siyo mke wangu na mtoto siyo wake.
“Niliendelea kumtaka anieleze sababu ya kutompeleka mtoto wetu hospitali ndipo aliposema ngoja anioneshe
Shangazi wa mtoto mchanga akikiuguza.
“Alitoka nje kumbe alikuwa anachemsha maji, alikuja nayo yakiwa kwenye sufuria aliloshika kwa kitambaa, akatumwagia mimi na mwanangu ambaye anajua hajui chochote,” alisema Mushi.
LENGO LAKE KUTUUA
Akaongeza:
“Naamini lengo lake lilikuwa ni kutuua na si vinginevyo. Ni jambo la
kusikitisha sana na majirani nao walisoneneshwa na tukio hili baya.
Muuguzi aliyejitambulisha kwa jina la Cristene Chilambo akimbeba mtoto huyo.
“Ni
vyema angesubiri niwe peke yangu, lakini alitumwagia maji akijua kuwa
nina mtoto tena mchanga. Nashukuru Mungu kwa sababu nilijitahidi kumkwepesha na maji yale ya moto, lakini yalimpata na kumuunguza kama unavyoona.”
AKIMBILIA POLISI
Mume huyo alisema: “Baada ya mke wangu kutufanyia kitendo kile alikimbilia polisi na kudai eti kuna mtu amemshambulia.
“lakini baadaye nilipopelekwa
polisi kuchukua PF 3 (hati ya kuruhusu nitibiwe), askari walishangaa
kuona nilivyounguzwa mimi na mwanangu na walipigwa na butwaa
nilipowaeleza kuwa aliyefanya hivyo ni mke wangu.
Mtuhumiwa Tunu Kimaro.
“Askari
polisi baada ya kupata ukweli ilibidi mke wangu awekwe ndani ili aweze
kutoa maelelezo ilikuwaje. Nashindwa kuelewa kama sababu ni kumlaumu kwa
kutompeleka hosptali mtoto wetu au kuna jambo lingine.
Post a Comment