Watanzania Mil 25 wanatumia vipodozi hatariWatanzania Mil 25 wanatumia vipodozi hatari
Asilimia
52 ya Watanzania wanawake kwa wanaume imedaiwa kuwa wanatumia vipodozi
ambavyo si salama kwa afya zao na ambavyo matumizi yake yamepigwa
marufuku nchini.
Baadhi ya vipodozi vilivyopigwa marufuku kutokana na kusababisha madhara ya kiafya.
Afisa
kutoka asasi ya Envirocare Bi. Ephrasia Shayo amesema hayo leo wakati
wa kampeni ya kuzuia matumizi ya vipodozi hatari inayoendeshwa na asasi
hiyo kwa kushirikiana na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA.
Bi. Ephrasia ametaja baadhi ya madhara yanayotokana na matumizi ya vipodozi hivyo kuwa ni saratanio ya ngozi, kuzaa watoto wenye ulemavu wa akili, kuharibika kwa mimba, maelezo ambayo yameungwa mkono na muelimishaji umma wa TFDA Bw. James Ndege.
Kwa mujibu wa Ndege, idadi kubwa ya vipodozi hivyo imeingia nchini kwa njia za panya kutokana na
hatua zinazochukuliwa na TFDA kudhibiti uingiaji wa vipodozi hivyo katika mipaka.
Amesema watu wengi wanakimbilia kunua vipodozi hivyo kutokana na kuuzwa kwa bei nafuu ambayo kila mwananchi anaweza kuimudu pasipo kujali madhara anayoweza kuyapata.
Muelimishaji huyo kutoka TFDA amewataka wananchi kuchukua tahadhari zote kuepuka matumizi ya vipodozi hatari, kama vile vyenye madini ya zebaki, hydroquinone na nyinginezo ambazo zikiingia mwililini zinaleta madhara makubwa kwenye viungo vya ndani ya mwili.

Post a Comment