Waathirika wa Mabomu Mbagala Walia na JK, Fidia walizolipwa Aibu!!!
Zaidi ya waathirika 1,000 wa milipuko ya mabomu Mbagala ya Aprili 2009 wamemuomba Rais Jakaya Kikwete
kuingilia kati na kuwasaidia ili waweze kupata fidia inayostahili.
Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu wa Kamati ya waathirika hao, Thomas
Mbasha alisema wamelipwa fidia ndogo na waliandika malalamiko yao kwa njia ya
maandishi kwa serikali wakitaka kuongezwa fidia lakini hawajapata majibu mazuri
hadi sasa.
“Tumeandika barua kadhaa kwa serikali tukiomba fidia zetu
lakini hakuna kilichofanyika… Tunahitaji Rais aingilie kati suala hili na
kutusaidia ili tulipwe stahili zetu kabla hajaondoka madarakani,” alisema.
Alisema fidia walizolipwa awali hazingulingana na thamani ya
mali na vitu walivyopoteza wakati wa mabomu hayo.
Waatjirika hao walionesha baadhi ya Hundi za benki zilzoikuwa
na kiasi cha shilingi 1,400/-, 2,700/-,
1,950/-, 4,900/- kiasi ambacho baadhi ya waathirika ndio walilipwa kama fidia
ya mali zao ikiwa ni pamoja na nyumba zilizokuwa zimeharibika kutoka na milipuko
ya mabomu hayo.
Hizi ndizo fedha zilizolipwa kaazi kwelikweli |
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Stephen Gimonge alisema Rais Kikwete
alitembelea eneo hilo na kuahidi kuhakikisha waathirika wanalipwa fidia
inayostahili lakini ahadi hiyo haijazaa matunda mpaka sasa.
“Alimuelekeza Waziri Mkuu kuhakikisha tunalipwa kulingana na
mali zetu zilizopotea… lakini malipo ya fidia yalipokuja wengine tulilipwa
chini ya kiwango” alisema na kusisitiza haja ya Rais Kikwete kuingilia kati na
kuwafikiria wale waliopewa hundi zenye kiasi kidogo na kuhakikisha waathirika
wote wanalipwa fidia zao.
Omary Mbonde ambaye ni mmoja wa waathirika hao alithibitisha
kulipwa Hundi ya fidia ya Sh 1,950/-.
“Fedha hizo nimelipwa kama fidia kwa ajili ya nyumba yangu
iliyoharibika pamoja na vitu vyangu vingine,” alisema na kuongeza kuwa
alipeleka malalamiko yake kwenye kamati ili apate fidia inayostahili lakini
hadi leo hajapata chochote.
Post a Comment