KUHUSU TUHUMA ZA KUMTAFUTIA MADEMU DIAMOND PLATINUMZ! AFUNGUKA QUEEN DARLEEN
“Unajua Naseeb miye ananiheshimu sana hata akiwa na wenzake kama alikuwa anaongea ujinga nikiwepo haongei kwakuwa anajua miye ni mkubwa wake,” Amesema Queen
“Na pia naweza kukaa hata miezi mitatu hatujaonana sasa nashangaa naambiwa namtafutia wanawake. Unajua sasa hivi yeye yupo juu na anafanya vizuri kwahiyo watu wanaongea tu vitu ambavyo hawavielewi."Siwezi kufanya hivyo hata siku moja kwani yeye ana maisha yake na uhuru wake na miye pia hivyo hivyo. Basi nisiwe na marafiki wazuri nitaambiwa namuunganishia mdogo wangu! Kwahiyo niwe sasa na marafiki vijuso sasa?
" Lazima watu wajue kuwa Diamond ni mdogo sana kwangu na tunaheshimiana sana siwezi kumpangia masuala ya mahusiano miye yeyote nitakayeletewa na yeye kwangu sawa ili mradi kampenda mwenyewe mie sina tatizo,” ameongeza.
Kwa upande mwingine muimbaji huyo amesema anatarajia kutoa wimbo aliomshirikisha mdogo wake huyo.
“Nipo busy sana na kazi zingine si unajua tena ila mashabiki wangu wasijali natoa wimbo mpya soon ambao nimemshirikisha mdogo wangu Naseeb aka Diamond Platnumz. Wimbo umefanyika kwa Tudd Thomas. Jina la wimbo bado sijajua. Sitowaangusha mashabiki wangu kama kawaida.”
Post a Comment