Header Ads

ARSENAL YAPATA SARE

 
Mfungaji wa bao la kwanza la Manchester City, Sergio Aguero dhidi ya Arsenal, alifunga bao hilo katika dakika ya 28.
 
Mshambuliaji wa Arsenal, Danny Welbeck (kushoto) akiwania mpira na mchezaji wa Manchester City, Frank Lampard.

 
Beki mkongwe wa Manchester City, Martin Demichelis (katikati) akiokoa hatari.
 
Beki wa Arsenal, Mathieu Debuchy akiwa chini baada ya kuumia mguu.
 
Mshambuliaji wa Arsenal, Danny Welbeck akiwa katika mshangao baada ya mpira aliopiga kugonga mwamba kisha kudakwa na kipa wa Man City, Joe Hart (hayupo pichani) katika kipindi cha kwanza.
 
Mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez akishangilia baada ya kuifungia timu yake bao katika dakika ya 74.
Mechi ya Ligi kuu ya England ‘Premiership’ kati ya Arsenal dhidi ya Manchester City imemalizika kwa sare ya mabao 2-2.
Wafungaji wa Arsenal ni Jack Wilshere dakika ya 63 na Alexis Sanchez (74) wakati Man City imepata mabao yake kupitia kwa Sergio Aguero dakika ya 28 na Martin Demichelis (83).

No comments

Powered by Blogger.