ROONEY AMFIKIA KWA MABAO THIERRY HENRY ENGLAND, SASA AWAFUKUZIA ANDY COLE NA SHEARER WANAOONGOZA
MSHAMBULIAJI
Wayne Rooney amemfikia kwa mabao gwiji wa Arsenal, Thierry Henry katika
Ligi Kuu ya England baada ya Nahodha huyo wa Manchester United kufunga
bao moja leo katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Queens Park Rangers.
Mchezaji huyo wa England alifunga dakika ya 44 na kufikisha jumla ya mabao 175 aliyofunga katika Ligi Kuu ya England pekee.
Mabao
mengine ya timu ya Louis van Gaal leo yamefungwa na Angel di Maria,
Ander Herrera na Juan Mata. Rooney sasa anashika nafasi ya tatu kwa
pamoja na Henry katika orodha ya wachezaji waliofunga mabao mengi Ligi
Kuu ya England kihistoria, nyuma ya Alan Shearer mwenye mabao 260 na Andrew Cole 187.
Nahodha huyo wa Manchester United akifunga dakika ya 44
Post a Comment