JAJA MTAMBO MPYA WA MABAO JANGWANI
MSHAMBULIAJI
Genilson Santana Santos ‘Jaja’ leo ameongeza heshima ya kocha Mbrazil,
Marcio Maximo baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa 3-0 kwenye
mechi ya Ngao ya Jamii, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Baadhi
ya viongozi wa Yanga SC hawakuridhishwa na uwezo wa mchezaji huyo na
wakaomba Maximo amkate, ili wasajili mchezaji mwingine watakayeona bora.
Lakini
jibu la Maximo lilikuwa ni kwamba, iwapo Jaja atakatwa naye ataondoka.
Maximo akawaambia viongozi wa Yanga SC kwamba Jaja ni mtaalamu wa
kufunga kama Toni Kroos wa Ujerumani na Bayern Munich.
Jaja akibusu Medali yake baada ya ushindi wa Ngao leo ulitokana na mabao yake mawili |
Jaja akiwa na kigogo wa Yanga SC, Seif Ahmed 'Magari' baada ya mechi |
Akasema
mashabiki wakitaka kuona chenga na madoido mengine ya kisoka
, wamtazame Haruna Niyonzima, lakini kwa mabao wasubiri kutoka kwa Jaja.
, wamtazame Haruna Niyonzima, lakini kwa mabao wasubiri kutoka kwa Jaja.
Yanga
SC wakawa wanaona kama Maximo anambeba Mbrazil mwenzake- lakini leo
Jaja amefunga mabao muhimu katika mechi muhimu, Yanga SC ikitwaa taji la
kwanza msimu wa 2014/2015.
|
Jaja
amefunga kipindi pili mabao mawili kabla ya Simon Msuva ‘kujazilizia’
ushindi huo kwa bao la tatu na sasa Yanga SC wanaelekea kwenye msimu
mpya wa Ligi Kuu wiki ijayo kwa furaha.
Baada
ya Jaja kufunga bao la kwanza, mashabiki wa Yanga SC wakaanza kuimba
jina lake- ajabu ni wale wale ambao baada ya Mbrazil huyo kumaliza
dakika 45 za kwanza bila kufunga walikuwa wakimzomea.
Mashabiki
wa Yanga SC wametoka Uwanja wa Taifa wakiimba jina la Jaja na sasa
wanaamini mchezaji huyo atawafunga na mahasimu wao Simba SC.
Ukweli
ni kwamba uchezaji wa Jaja ‘kivivu’ unakatisha tamaa mapema, lakini kwa
kitendo cha kufunga mabao manne ndani ya mechi tano- anaweza akawa
kweli mkali wa mabao kama asemavyo Maximo.
SOURCE: BIN ZUBEIRY
Post a Comment