PICHA: BALAA LA FIESTA SHINYANGA
TAMASHA la
Serengeti Fiesta 2014, usiku wa kuamkia leo lilifunika mbaya kutokana
na mashabiki kibao kujitokeza kwa wingi ndani ya uwanja mdogo wa
Kambarage, Shinyanga ambapo kila msanii aliyepanda, alipata shangwe za
kutosha.
Mpango mzima
ulikuwa hivi, msanii wa kwanza kulitawala jukwaa alikuwa ni Mo Muziki,
ambaye alipata shangwe za hatari na baadaye alishuka na kumkabidhi
kipaza sauti mwanadada Khadja anayesumbua na wimbo wa Maumivu ambaye pia
alikamua vilivyo na kumwachia jukwaa Recho kisha kumpisha Young Killer.
Makamuzi
yalizidi kushika kasi baada ya Ommy Dimpoz kupanda jukwaani na
kumkaribisha mrembo mmoja ambaye walijiachia vilivyo na kumpa pasi
Stamina ambaye alikamua na kumuachia jukwaa Nay wa Mitego aliyempisha
mtangazaji, Adam Mchomvu ambaye alimpandisha mwanadada Linah.
Shangwe
zilikolea zaidi baada ya Mr Blue kupanda na baadaye kuwapisha Chegge na
Temba ambao nao walifanya shoo kali na kumpisha Nikki wa II ambaye
alifanya yake na kumpa kipaza Fid Q ambaye alifunga pazia burudani hizo.
(PICHA/HABARI NA MUSA MATEJA/GPL)
Post a Comment