Header Ads

WEMA, DIAMOND, AUNT WANATAJWA KWENYE MICHEPUKO HATARI!



Mastaa watatu Bongo, Wema Isaac Sepetu, mpenzi wake Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Aunt Ezekiel wakiwa katika picha ya pamoja.

NI TAMAA YA NGONO AU NI NINI? HIVYO NDIVYO UNAVYOWEZA KUJIULIZA BAADA YA KUBAINIKA KWAMBA MASTAA WATATU BONGO, WEMA ISAAC SEPETU, MPENZI WAKE NASIBU ABDUL ‘DIAMOND PLATNUMZ’ NA AUNT EZEKIEL GRAYSON WANATAJWA KWENYE MCHEPUKO HATARI WA KUZUNGUKANA KIMALOVEE, IJUMAA LINA KILA SABABU YA KUKUJUZA.

KILA KUKICHA
Ishu hiyo imebumburuka baada ya hivi karibuni mastaa kutengeneza vichwa vya habari kila kukicha kuhusiana na mambo yao hayo.
AUNT NA MOZE IYOBO
Duru za kihabari zinaonesha kwamba hivi karibuni mwigizaji Aunt, bila ya kupepesa macho huku akijua dhahiri kuwa ni mke wa mtu, Sunday Demonte alifungua kinywa na kuapa kuwa hawezi kuachana na mume wa mtu, Moses Peter Iyobo ‘Moze Iyobo’ ambaye ni densa wa Diamond.
Aunt alitamka maneno hayo akijua fika kuwa Moze Iyobo ni mume wa mwanamke aitwaye Mwengy ambapo wanaishi Mbagala jijini Dar, wakiwa wamejaliwa mtoto mmoja.
Mume wa mtu, Moses Peter Iyobo ‘Moze Iyobo’ akiwa na ‘Diamond Platnumz’.

No comments

Powered by Blogger.