Mwili wa marehemu Mussa ukiwa
katika chumba cha kuhifadhia
maiti katika hospitali ya mkoa wa
Shinyanga wakati wa kufanyiwa
postmoterm leo
Kijana mmoja aliyejulikana kwa
jina la Mussa Shija mkazi wa kata
ya Chibe katika manispaa ya
Shinyanga ameuawa kwa kupigwa
kitu kizito kichwani na watu
wasiofahamika akiwa kwenye
tamasha la Serengeti Fiesta
lililokuwa linafanyika usiku wa
kuamkia leo katika uwanja mdogo
wa Kambarage mjini Shinyanga
Akizungumza na KITAANI BONGO NEWS
mganga mfawidhi wa hospitali ya
mkoa wa Shinyanga Dkt Fredrick
Mlekwa amesema uchunguzi wa
kitaalam walioufanya unaonesha
kuwa kijana huyo alipigwa na kitu
butu kichwani na kusababisha
kuvuja damu kichwani kutokana
na kuvunjika kwa fuvu la kichwa.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa
wa Shinyanga Mussa Athuman
amethibitisha kutokea kwa tukio
hilo na kuongeza kuwa uchunguzi
wa awali unaonesha kuwa kijana
huyo aliuawa kwa kushambuliwa
na watu wasiojulikana nje ya fensi
la uwanja mdogo wa Kambarage
palipokuwa panafanyika tamasha
la Fiesta.
Hata hivyo amesema jeshi la
polisi litatoa taarifa kamili
baadaye kwani linaendelea.
source: Kitaano Bongo
Post a Comment