Header Ads

VALENCIA ATOA BURUDANI, APIGA BAO TAAMUUU


Mshambuliaji Enner Valencia wa West Ham amefunga bonge la bao katika mechi ya Ligi England dhidi ya Hull City, jana.

Mechi hiyo ilimalizika kwa sare ya mabao 2-2 huku yote manne yakionekana kuwa “bonge” ya mabao.
Lakini lile la Valencia alilofunga kutokana na shuti lake la umbali wa yadi 20 lilikuwa kali zaidi.
Shuti lake lilichukua muda wa sekunde 7 tu kuwa limetinga nyavuni tokea alipokuwa yeye.
Pia kasi yake ilionekana kuwa kubwa zaidi kwani ilikuwa ni mita 70.1 kwa saa.

No comments

Powered by Blogger.