UKWELI KUHUSU: Juma Nature kufanya collabo na Wanaume Family
Miaka
kadhaa imepita tangu kundi la Wanaume TMK livunjike na kuzaa makundi
mawili ya Wanaume Family na Wanaume Halisi ambayo kwa kipindi cha nyuma
yalionekana kuwa na uhasama.
Rapper/mwimbaji
mkongwe wa TMK, Juma Nature amezungumza na tovuti ya Times Fm kuhusu
uwezekano wa kuipata ladha mchanganyiko ya collabo kati ya wasanii wa
makundi hayo mawili.
“Inawezekana
hiyo ni mipango. Hauwezi kusema kwamba kitu fulani kwamba kitafanyika
tu, hapana. Hiyo ni mipango tu.” Juma Nature ameiambia tovuti ya Times
Fm.
“Inategemea
kazi zenu zinaendaenda vipi, mko karibu? Kwa sababu kila mmoja sasa
hivi ana familia yake ujue. Huwezi kumchukua huyu kwenye familia yake
ukamwambia tufanye hili wakati kila mmoja ana kundi lake.” Ameongoza.
Amefafanua kuwa hakuna mwiko wowote kati ya wasanii wa kundi lake kufanya kazi na wasanii wa kundi lolote lile.
“Hakuna mwiko wowote yaani, kazi zinafanyika tu kwa kuwa wote wanajua sanaa na wote ni watu wa watu.”
SOURCE:Times fm
Post a Comment