SAMAHANI KWA PICHA HIZI: [ZINATISHA] ANYONGWA NA MPENZI WAKE NA KUTUPWA KORONGONI HUKO KIGOMA!

Baba mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Kaga mkazi wa Mwanga Kisangani ''B'' jirani na Saigoni amemuua mpenzi wake kwa kumnyonga na kumtumpa katika makorongo ya Kilimahewa ''B'' Chini ya Shule ya Msingi Kilimahewa.
Taarifa
za awali zinasema kulikuwa na ugomvi baina yao hao wapenzi wawili hali
iliyopelekea mwanamke (Mama Koku) kumshtaki mwanaume mahakamani na
kusababisha Mwanaume kufungwa miezi miwili jela. Siku
kadhaaa baada ya mwanaume kutoka gerezani alipata habari kuwa mpenzi
wake huyo aliyesababisha kuwekwa ndani anatembea na mwanaume mwingine
ndipo mwanaume huyo alipopanga njama/namna ya kutekeleza mauwaji hayo.
Taarifa zinasema mara baada ya
mwanaume kudhamiria kutekeleza tukio hilo lililo kinyume na neno la
MUNGU katika kitabu kile cha Kutoka 20.13 alimwambia mpenzi wake
kuwa; "Leo nimejisikia tutoke out twende Beach za Gorden tukajivinjari"
Mwanamke (Mama Koku) bila shaka lolote aliongozana nae mpenzi wake huyo
ndipo wakiwa njiani katika makorongo ya Kilimahewa ''B'' mwanaume
alimbadilikia ghafla na kumkaba kooni mwanamke na kupelekea kupoteza
maisha.
Post a Comment