PIGO LINGINE UKUTA WA MAN UNITED, PHIL JOSEN NJE WIKI TATU
PIGO lingine
katika safu ya ulinzi ya Manchester United, baada ya Phil Jones kuumia
akiichezea England dhidi ya Uswisi Jumatatu mechi ya kuwania tiketi ya
Euro 2016 na sasa atatakiwa kuw anje kwa wikihadi tatu.
Beki
huyo wa Manchester United amekuwa chini ya uangalizi wa timu ya
madaktari ya klabu tangu amerejea kutoka Basle, ambako alicheza kwa
dakika 77 kabla ya kumpisha Phil Jagielka.
Kulikuwa
kuna wasiwasi kwamba Jones anaweza kuwa nje kwa mwezi mmoja, lakini
vipimo vimeonyesha anaweza kuwa nje kwa wiki mbili hadi tatu.
Phile Jones alikuwemo kwenye kikosi kilichoshinda 2-0 dhidi ya Uswisi mjini Basle
Jones
wazi sasa atakosa mechi za Manchester United dhidi ya QPR Uwanja wa Old
Trafford Jumapili ambako wachezaji wanne wapya wanawexa kuanza
kuitumikia klabu hiyo.
Radamel
Falcao na Daley Blind walitambulishwa jana kama wachezaji wapya wa
klabu hiyo na wanaweza kuungana na wenzao wengine wapya, Luke Shaw na
Marcos Rojo.
Kocha
Louis van Gaal bado anasotea ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu England,
baada ya mwanzo mbaya ambao imeshuhudiwa akiambulia pointi mbili tu
huku akitolewa na timu ndogo MK Dons katika Kombe la Ligi, maarufu
Capital One Cup.

Post a Comment