Lesotho Yaomba Walinda Amani wa SADC
Waziri Mkuu huyo anashtumu jeshi na naibu Waziri Mkuu Mothetjoa Metsing kwa njama za kumtimua madarakani
Waziri Mkuu wa Lesotho ameomba walinda amani wa kusini mwa Afrika kupelekwa nchini mwake kufuatia kile anachosema ni mapinduzi ya serikali yaliyofanyika mwishoni mwa wiki.
Msaidizi wa Thomas Thabane, alisema Waziri Mkuu huyo aliomba msaada huo wakati wa mkutano wa dharura na maafisa wa Jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika Jumatatu mjini Pretoria.
Msaidizi huyo Samonyane Ntsekele, aliwaambia waandishi habari kuwa mzozo huo unahitaji kuingiliwa kati. Bw.Thabane alitoroka Lesotho Jumamosi kabla ya jeshi kuzingira makao yake na yale ya afisa wa ngazi ya juu wa polisi, ambapo pia waliwapokonya silaha askari polisi katika vituo viwili vya polisi mjini Maseru.
Waziri Mkuu huyo anashtumu jeshi na naibu Waziri Mkuu Mothetjoa Metsing kwa njama za kumtimua madarakani.
SOURCE: SAUTI YA AMERIKA
Post a Comment