Header Ads

CAMEROON MPYA YAIFUMUA IVORY COAST 4-1 YAYA TOURE NDANI, UGANDA YASHINDA MBIO ZA AFCON


 Cameroon imeichakaza Ivory Coast kwa mabao 4-1 katika mechi ya kuwania kucheza Kombe la Maita Afrika.
KIKOSI kipya cha Cameroon kimeendeleza wimbi la ushindi katika kuwania tiketi za Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani Morocco, baada ya jana kuifumua Ivory Coast mabao 4-1 mjini Yaounde.
Clinton N'Jie na Vincent Aboubakar kila mmoja alifunga mabao mawili kwa Simba Wasiofungika huku bao pekee la Tembo wa Ivory Coast likifungwa na Mwanasoka Bora Afrika, Yaya Toure.
Baadhi ya wachezaji nyota wa Ivory Coast kama nahodha Yaya Toure, kiungo wa Newcastle, Cheikh Tiote na mshambuliaji wa Swansea, Wilfried Bony walikuwa kwenye kikosi hicho kilichotandikwa.

Bahati nyingine mabya kwa Ivory Coast, beki wake Serge Aurie anayekipiga PSG alilazimika kukimbizwa hospitali baada ya kugongana na mshambuliaji wa Cameroon.
Yaya amesema wanalazimika kushinda mechi zote zilizobaki kuinua upya matumaini ya kucheza michuano hiyo ya Afrika.




MATOKEO KUFUZU AFCON JANA; 

Kundi A
Kongo 2-0 Sudan 
Afrika Kusini 0-0 Nigeria 
Kundi B
Malawi 3-2 Ethiopia
Algeria 1-0 Mali
Kundi C
Angola 0-3 Burkina Faso
Lesotho 1-1 Gabon
Kundi D
Cameroon 4-1 Ivory Coast 
Sierra Leone 0-2 DRC
Kundi E
Togo 2-3 Ghana
Uganda 2-0 Guinea
Kundi F
Cape Verde 2-0 Zambia
Msumbiji 1-1 Niger
Kundi G
Misri 0-1 Tunisia
Botswana 0-2 Senegal












Cameroon iliyosukwa upya baada ya Kombe la Dunia, ilishinda mechi ya kwanza ya Kundi D mabao  2-0 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Jumamosi iliyopita.
Cameroon, Algeria, Kongo Brazzaville, Burkina Faso, Cape Verde, Senegal na Tunisia zimefanikiwa kushinda mfululizo mechi mbili za mwanzoni wakati Misri ina hali mbaya baada ya kufungwa mfululizo.
Mabingwa watetezi Nigeria wameendeleza rekodi ya kutofungwa na kuruhusu nyavu zao kuguswa na Afrika Kusini, baada ya kulazimisha nao sare ya bila kufungana 0-0 mjini Cape Town.
Super Eagles walipambana mno kupata sare hiyo ugenini, baada ya kupoteza mechi ya kwanza nyumbani mbele ya Kongo Jumamosi iliyopita.
Uganda imeifunga 2-0 Guinea, Algeria imeshinda 1-0 dhidi ya Mali mjini Blida, Kongo imeifunga Sudan 2-0 mjini Pointe-Noire, Burkina Faso imeichapa Angola 3-0 mjini Luanda na Cape Verde imewafunga mabingwa wa 2012 Zambia 2-1 mjini Praia.

Senegal imeshinda 2-0 dhidi ya Botswana mjini Gaborone na Tunisia imewafunga mabingwa wa kihistoria Misri 1-0 mjini Cairo, wakiwaacha Mafarao bila pointi katika Kundi G.

No comments

Powered by Blogger.