BALOTELLI HAISHI VITUKO, AVUA JEZI, BUKTA AKIWA MAZOEZINI!
| ETI ALIVUA HIVI KWA KUWA ALIKUWA ANAVAA VIZURI, HIVYO ALITAKA ACHOMEKEE...BALOTELLI WA INTER MILAN, MAN CITY, AC MILAN NA SASA LIVERPOOL, VITUKO PALEPALE TU! ILA JAMAA BURUDANI SANA. |
Licha ya vituko hivyo pia, Liverpool ilifanikiwa
kuingiza pauni 50,000 kupitia mauzo ya jezi za Mario Balotelli, siku ya kwanza
tu baada ya kumsajili.
Balotelli ,24, amejiunga na
Liverpool akitokea AC Milan kwa kitita cha pauni milioni 16.
Mashabiki wa Liverpool
wakampokea wakionyesha wanamkubali wakinunua jezi zake kwa wingi na kuiingizia
klabu yao pauni 50,000 ambayo ni rekodi kwa mauzo ya siku moja.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Liverpool, Ian Ayre amethibitisha hilo na kuonyesha nguvu ya mashabiki wa klabu
hiyo kongwe yenye mashabiki wenye moyo wa chuma.
Mtaliano huyo alifunga mabao 20 katika mechi 54 akiwa na Manchester City katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2013 alipoondoka kwenda AC Milan.



Post a Comment