JOPO LA MAJAJI KWA AJILI YA KUMTAFUTA MSHINDI WA TUZO YA RAIS YA HUDUMA ZA JAMII NA UWEZESHAJI YAFANYA ZIARA KATIKA MIGODI YA BULYANHULU NA BUZWAGI
Mkurugenzi
Mtendaji wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu Gold Mine Bw. Peter Burger (
wa kwanza kushoto) akizungumza na jopo la majajaji na sekretarieti
iliyotembelea mgodi huo kwa ajili ya kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais
ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji.
Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Msingi ya Ibanza Bw. Dions Kagiye (katikati)
akizungumza na baadhi ya majaji waliotembelea shule hiyo inayofadhiliwa
na mgodi wa Bulyanhulu Gold Mine kwa ajili ya kuifanyia tathmini.
Mmoja
wa majaji Dkt. Yohana Mtoni (kushoto) akimsaidia mmoja wa watoto
waliofika katika
kisima cha maji cha Ilogi kuvuta maji. Kisima hicho
kinafadhiliwa na mgodi wa Bulyanhulu
Meneja
Mahusiano wa Mgodi wa Buzwagi uliopo Kahama, Shinyanga Bi. Dorothy
Bikurakule ( wa kwanza kulia mbele) akiongoza jopo la majaji na
sekretarieti kutembelea kituo cha afya cha Mwendakulima kinachofadhiliwa
na mgodi huo.
Meneja
Mahusiano wa Mgodi wa Buzwagi uliopo Kahama, Shinyanga Bi. Dorothy
Bikurakule (katikati) akielezea mchango wa mgodi huo katika uwezeshaji
wa kikundi cha vijana cha ufyatuaji wa matofali cha Mwendakulima.
Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mwendakulima Bi. Diana Kuboja akielezea
mchango wa mgodi wa Buzwagi Gold Mine katika ujenzi wa shule hiyo kwa
majaji na sekretarieti iliyotembelea shule hiyo kwa ajili ya kufanya
tathmini.
Post a Comment