Arsenal Hofu yatanda kuumia kwa Debuchy
KLABU
ya Arsenal ipo katika hofu kubwa baada ya beki wake wa kulia Mathieu
Debuchy ameumia vibaya na haijajulikana bado atakaa nje ya kiwanja kwa
muda gani .
Kocha Arsene Wenger amesema majeraha
ya Debuchy’s ‘Hayaonyeshi' kupona upesi na kuna hitajika kufanyika
uchunguzi wa kina zaidi waweze kugundua atakaa nje kwa muda gani .
Mchezaji huyo alianguka vibaya na kukanyaga kifundo chake cha mguu wa kushoto
katika kipindi cha pili cha mchezo kati ya Arsenal na Manchester City ulioisha kwa sare ya 2-2.
Debuchy, 29 alijiunga na
Arsenal katika majira ya kiangazi akichukua nafasi ya Bacary Sagna,aliyejiunga na Man City, na alicheza vizuri katika mechi
na klabu yake ya zamani katika uwanja Emirates.
Post a Comment